Pages - Menu

Sunday, April 19, 2015

Njia TATU za uhakika za kufikia utajiri (Ajira sio Mojawapo)

1. Biashara
Hii ni njia ya kwanza ya uhakika ya kufikia uhuru wa kifedha. Katika biashara unaweza kutengeneza au kutafuta soko la bidhaa, huduma au hata mawazo yanayoweza kuboresha kitu. Biashara inakuwezesha wewe kutumia nyenzo ya muda wa watu wengine, fedha za watu wengine na hata utaalamu wa watu wengine kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Aina ya biashara tunayozungumzia hapa ni biashara kubwa ambayo haikuhitaji wewe kila mara ndio iweze kwenda vizuri/ Kama bado hujaingia kwenye biashara anza sasa mchakato wa kuangalia ni biashara gani unayoweza kufanya. Kabla hujaingia kwenye biashara yoyote hakikisha inauwezo wa kukua na kuendeshwa bila ya wewe kuwepo moja kwa moja.

2. Uwekezaji
Hii ni njia nyingine muhimu ya kuweza kujitengenezea kiasi kikubwa cha fedha na hivyo kufikia uhuru wa kifedha. Katika uwekezaji unaweza kuwekeza fedha zako katika hisa, vipande na hata mifumo mingine ya uwekezaji wa fedha. Uzuri wa uwekezaji ni kwamba wewe unawekeza tu fedha zako na kuwa mfuatiliaji, huhitaji kufanya kazi moja kwa moja, bali fedha yako ndio inakufanyia kazi.

Kila mtu anaweza kuwa muwekezaji mzuri kama atapata elimu husika juu ya uwekezaji.

3. Umiliki wa mali
Njia nyingine unayoweza kuitumia kufikia utajiri ni umiliki wa mali. Unaweza kununua ardhi na kukaa nayo na jinsi siku zinavyokwenda thamani yake inaongezeka. Pia unaweza kujenga nyumba kwa ajili ya biashara yaani kuuza au kupangisha. Kwa njia hizi unatumia mali unazomiliki kutengeneza fedha zaidi.

Angalizo muhimu kwa njia hizi nne
Sio kwamba ukishaingia tu kwenye moja ya njia hizi TATU basi tayari wewe ni tajiri. Unahitaji kufanya kazi kwa bidii na maarifa na pia unahitaji uvumilivu mkubwa kwa sababu changamoto ni nyingi sana na zinaweza kukukatisha tamaa.

Pia jinsi unavyoanza mapema ndio unavyojiwekea nafasi nzuri ya kufikia utajiri mapema. Mtu anayeanza biashara au uwekezaji akiwa na miaka 30 ni tofauti kabisa na mtu anayeanza akiwa na miaka 40 au 50. Jitahidi uanze sasa bila ya kujali umri ulionao.

Muhimu zaidi ni kwamba unaweza kuzitumia njia zote. Sio kwamba ukishatumia njia moja basi nyingine huruhusiwi, hapana, unaweza kutumia zote unavyotaka mwenyewe. Kwa mfano unaweza kuwa na biashara ambayo pia umeiweka kwenye mtandao na faida unayopata kwenye biashara zako unaiwekeza kwenye biashara hiyo na kwenye aina nyingine za uwekezaji na pia unanunua mali zaidi.

Kwa nini ajira haiwezi kukufikisha kwenye utajiri?
Naamini mpaka sasa utakuwa umeshajua kwa nini ajira haiwezi kukufikisha kwenye utajiri. Kama bado hujajua sababu ni kwamba kwenye ajira kipato chako kinaamuliwa na watu wengine. Hata ukifanya kazi kwa juhudi na maarifa kiasi gani bado kipato chako huwezi kuamua mwenyewe.

Sababu nyingine inayofanya ajira isiweze kukufikisha kwenye utajiri ni kwamba kwenye ajira unatumia muda wako tu ili kupata fedha. Wakati kwenye biashara na uwekezaji mwingine unaweza kutumia muda wa watu wengine kujizalishia wewe fedha. Jinsi unavyoweza kuwatumia watu wengi zaidi kukuzalishia ndivyo unavyoweza kufikia utajiri mapema.

0 comments:

Post a Comment